• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yasaka wawekezaji katika sekta ya dijitali na miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2019-07-10 19:10:25

    Serikali ya Rwanda imeanza mikakati ya kutafuta wawekezaji katika sekta ya digitali na maendeleo ya miundo mbinu kwenye mkutano wa kila mwaka wa Africa 50. Mkutano huo ambao unahudhuriwa na nchi 27 kutoka Afrika serikali ya Rwanda imesema hiyo ndio nafasi wanalenga kutumia kuonyesha fursa zilizopo katika maeneo mbali mbali nchini humo. Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na miundo mbinu katika mji mkuu wa Kigali.Rwanda imekuwa ikishirikiana kwa karibu na sekta ya kibinafsi katika kufanikisha maendeleo ya kiuchumi nchini humo.Hivi sasa Rwanda ndio nchi ambayo imekuwa ikisifiwa kwa kiasi kikubwa katika kuweka mazingira bora ya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako