• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa Uingereza nchini Marekani ajiuzulu kutokana na mgogoro uliotokana na kuvuja kwa ujumbe wa kumpinga rais wa Marekani

  (GMT+08:00) 2019-07-11 09:01:56

  Balozi wa Uingereza nchini Marekani Bw. Kim Darroch amejiuzulu wakati mgogoro wa kidiplomasia ukiendelea kutokana na kuvuja kwa ujumbe wa kumkosoa rais Donald Trump wa Marekani.

  Katika barua yake ya kujiuzulu aliyomwandikia mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza Bw. Simon McDonald, Darroch amesema, tangu kuvuja kwa nyaraka ya kiserikali kutoka ubalozi huo mjini Washington, kumekuwa na fikra mbalimbali kuhusu wadhifa wake. Amesema kutokana na hali ya sasa ni vema kwa balozi mwingine mpya akateuliwa kuchukua nafasi yake.

  Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May ameliambia baraza la chini la bunge kuwa baraza lake la mawaziri lina Imani na Bw. Darroch kama balozi wa nchi hiyo huko Washington, na kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya balozi huyo ya kujiuzulu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako