Kulingana na Njoroge, kampuni hizi huenda zinatoa fursa na kuwachochea walaghai kusambaza pesa ghushi kwa wananchi. Gavana wa Benki kuu alitoa mfano wa mashirika ya Tala, Branch na Okash ambayo yanatumiwa sana na wakenya kukopa pesa, huenda yakatumiwa vibaya na walaghai kusambaza pesa ghushi. Mkuu huyo amesema kwamba lengo kuu la kukagua kampuni hizi ni kubaini wapi zinatoa pesa hizi za kuwapa wananchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |