Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Marjolijn Sonnema, alisema mpango huo utafanikishwa kupitia maofisa ugani nchi nzima. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alisema mkataba huo una maana kubwa kwa Tanzania kama nchi kwani utaongeza uzalishaji na kuinua maisha ya mfugaji. Alisema Tanzania inavuna kiasi cha tani 350,000 za samaki kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji halisi ya tani 700,000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |