• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuharakisha matumizi ya teknolojia ya juu katika mambo ya bandari

    (GMT+08:00) 2019-07-11 19:12:04

    Leo tarehe 11, Julai ni siku ya safari ya baharini ya China. Naibu waziri mawasiliano ya mawasiliano na uchukuzi wa China Bw. Liu Xiaoming amesema, China imeshika nafasi ya kwanza duniani kwa uwezo wa kupakia na kupakua mizigo na makontena bandarini kwa miaka 16 mfululizo, hata hivyo China bado haina nguvu kubwa katika usafirishaji wa bidhaa baharini. Ameongeza kuwa China itaharakisha matumizi ya teknolojia mpya za juu katika mambo ya bandari.

    Katika miaka ya hivi karibuni, China imekamilisha mfumo wa kisasa wa usafirishaji wa bidhaa baharini, kwa kujenga bandari nyingi katika sehemu za pwani. Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa China Bw. Liu Xiaoming anasema,

    "Kati ya bandari 10 zenye uwezo mkubwa zaidi wa kupakia na kupakua mizigo na makontena duniani, bandari 7 ziko China. Kiasi cha usafirishaji wa bidhaa baharini cha China kinachukua theluthi moja ya kiasi hicho cha jumla cha dunia nzima. Meli za China zinasafiri kati ya China na nchi nyingine zaidi ya 100, na China ina mtandao wa huduma za usafirishaji wa bidhaa babarini kote duniani."

    Hata hivyo, Bw. Liu amesema China bado si nchi yenye nguvu zaidi ya usafirishaji wa bidhaa baharini, hivyo itaharakisha matumizi ya teknolojia mpya za juu katika mambo ya bandari zikiwemo akili bandia, 5G, mfumo wa utambuzi wa mahali kwa satilaiti wa Beidou.

    Katibu mkuu wa Shirika la kimataifa la Mambo ya Baharini Bw. Kitack Lim amesema China inafanya kazi muhimu katika kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia za usafirishaji baharini na maendeleo yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira. Anasema,

    "Shirika letu linajitahidi kutatua masuala ya teknolojia za meli za kujiendesha na matumizi ya nishati safi. China inatoa mchango katika suala hilo. Kwa mfano tumeshirikiana na kuanzisha kituo cha utafiti wa teknolojia za mambo ya baharini katika Chuo Kikuu cha Mambo ya Baharini ya Shanghai."

    Naibu waziri wa mawasiliano ya barabara na uchukuzi wa China Bw. Liu amesema, China pia itahimiza mawasiliano na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika mambo ya baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako