• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la China lapinga vikali Marekani kuuza silaha kwa Taiwan

    (GMT+08:00) 2019-07-11 19:31:54

    Msemaji wa wizara ya ulinzi wa China Bw. Wu Qian amesema, Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China. Jeshi la China linapinga vikali Marekani kuuza silaha zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.22 kwa Taiwan.

    Bw. Wu amesema kitendo hicho kisicho sahihi cha Marekani kimekiuka mamlaka na usalama wa China na kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kuingilia mambo ya ndani ya China na kuvuruga maendeleo ya uhusiano wa kijeshi kati yao na amani na utulivu wa mlangobahari wa Taiwan.

    Bw. Wu amesisitiza kuwa suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China na linahusiana na maslahi makuu ya China na hisia za kitaifa za watu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako