• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchambuzi: ongezeko la uwekezaji wa kigeni nchini China laonyesha kuwa kampuni za nje zina imani na uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2019-07-11 19:47:14

    Takwimu zilizotolewa leo na Wizara ya Biashara ya China zinaonyesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya mitaji ya kigeni iliyotumiwa nchini China ilifikia dola za kimarekani bilioni 70, kiasi ambacho kiliongezeka kwa asilimia 7.2 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho. Wakati hatari ya uchumi wa dunia inaongezeka, na kasi ya ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni duniani inapungua, uwekezaji wa kigeni nchini China unaendelea kuongezeka, na hii imeonyesha kuwa kampuni za nje zina imani na uchumi wa China.

    Sifa mbili kuu zimeonekana katika uwekezaji wa kigeni nchini China. Kwanza, uwekezaji huo unakwenda katika sekta zenye teknolojia ya juu kutoka sekta za usindikaji. Pili, nchi zinazotokea kampuni hizo zinaendelea kuwa zile zile, na kwamba uwekazaji kutoka Korea Kusini, Japan, Ujerumani na Umoja wa Ulaya uliongezeka kwa asilimia 63.8, asilimia 13.1, asilimia 81.3 na asilimia 22.5 mtawalia.

    Je, ni kwa nini kampuni kutoka nchi hizo zinaongeza uwekezaji wao nchini China? Sababu ni kuwa, kwanza, China ina watu bilioni 1.4 na idadi kubwa ya watu wenye kipato cha kati ambao wanaunda soko kubwa na kutoa faida halisi kwa kampuni hizo. Pili, katika makadirio ya uchumi wa dunia yaliyotolewa na Benki ya Dunia mapema mwezi Juni, makadirio kuhusu ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu na mwaka kesho yalishushwa lakini yale kuhusu uchumi wa China hayakubadilika, na Benki hiyo inaona China ina uwezo wa kukabiliana na changamoto kutoka nje. Tatu, dhamira ya China kuendelea kufungua mlango na kuboresha mazingira ya kibiashara imezipatia imani kampuni hizo za nje.

    Wakati sera ya kujilinda kibiashara inaendelea duniani, uwekezaji wa kigeni hauondoki bali kuongezeka nchini China, hii inaonyesha kuwa wawekezaji wa nje wamegundua kuwa uchumi wa China unaotafuta maendeleo bora ni fursa kubwa kwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako