• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFCON: Timu zote za nusu fainali zapatikana, ni kivumbi kati ya Nigeria dhidi ya Algeria na Senegal dhidi ya Tunisia

    (GMT+08:00) 2019-07-12 10:07:59

    Hayawi hayawi ndio yanaanza kuwa kidogokidogo baada sasa kupata timu zote zitakazotinga nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika. Tunisia ilifika katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza tangu 2004 baada ya kuilaza Madagascar. Mwewe hao wa Carthage, ambao sasa watapambana na Senegal siku ya Jumapili katika nusu fainali waliongoza kupitia bao la Ferjani Sassi. Youssef Msakni baadaye alifunga goli la pili baada ya shambulio la Wahbi Khazri kupanguliwa na Melvin Adrien. Naim Sliti aliipatia Tunisia bao la tatu katika muda wa lala salama na kuwakata makali wachezaji wa Madagascar ambao walikuwa wakilivamia lango la Tunisia kama nyuki waliotoka katika mzinga. Wakati huohuo Algeria ilitinga nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuilaza Ivory Coast 4-3 kupitia penalti baada ya sare ya 1-1 baada ya muda wa zaida. Algeria ilianza kuwa kinara kupitia winga wa zamani wa klabu ya West Ham Sofiane Feghouli kabla ya kupoteza mkwaju wa penalti. Baghdad Bounedjah ambaye alikuwa amechezewa rafu katika lango la Ivory Coast aligonga mwamba wa goli alipozawadiwa penalti hiyo. Ivory Coast ililazimisha muda wa ziada baada ya mshambuliaji wa Aston Villa Jonathan Kodja kufunga bao zuri. Na baada ya sare hiyo uamuzi wa kupiga penalti ulitolewa. Algeria ambayo inatafuta ushindi wa kwanza wa kombe hilo tangu 1990 sasa itakutana na Nigeria mjini Cairo siku ya Jumapili. Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha alipewa kadi ya njano baada ya kuzua mgogoro na Bensabaini. Mchezaji huyo wa Ivory Coast na mshambuliaji wa Algeria Riyad Mahrez walitolewa kufikia mwisho wa dakika 120 na hawakushiriki katika upigaji wa penalti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako