• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ndairagije ateuliwa kuwa kocha wa muda Taifa Stars

    (GMT+08:00) 2019-07-12 10:09:07

    Kocha Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa muda wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kushika nafasi ya Emmanuel Amunike aliyetimuliwa. Uteuzi wa Ndayiragije ambaye kwa sasa yuko nchini Rwanda akiiongoza Azam FC kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) umetangazwa jana mara baada ya kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukutana kwa dharura jijini Dar es Salaam. Etienne akiwa na KMC katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kukiwezesha kikosi hicho kupata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho la CAF pamoja na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA. Kocha huyo ambaye atakiongoza kikosi hicho katika michezo ya kuwania kufuzu mashindano ya CHAN, amependekeza benchi lake la ufundi kusaidiwa na kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda pamoja na kocha msaidizi wa Pokisi Tanzania, Seleman Matolab ambao uteuzi huo umezingatia programu maalum ya kuendeleza makocha wazawa.

    Wakati huohuo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uganda (FUFA) limemteua Abdallah Mubiru kuwa kocha wa muda wa Uganda Cranes. Mubiru anachukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa Cranes Sebastien Desabre ambaye mkataba wake ulikatizwa na kujiunga na klabu ya Pyramids FC ya Misri. Mubiru atasaidiwa na Livingstone Mbabazi na Sadiq Wasswa kama makocha wasaidizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako