• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASUMBWI: Kocha Freddie Roach asema Pacquiao anaweza kurudiana na Mayweather

  (GMT+08:00) 2019-07-12 10:10:44

  Mwalimu wa ngumi, Freddie Roach amesema kuwa anategemea Manny Pacquiao anaweza kupanga pambano la marudiano dhidi ya Floyd Mayweather baada ya gwiji huyo wa Phillipines kuamua kupambana na Keith Thurman jijini Las Vegas mwezi huu. Roach aliwaambia waandishi wa habari kuwa bado anakerwa na kipigo ambacho Pacquiao alipata kwa Mayweather katika pambano la mwaka 2015, ambalo lilitangazwa kama "Pambano la Karne" lakini likaishia kwa kukera mashabiki. Baadaye Pacquiao alisema jeraha la bega alilokuwa nalo lilimzuia kupambana kwa kiwango chake katika pambano hilo la raundi 12, wakati Mayweather alitangaza kustaafu mwaka huo akiwa na rekodi ya kutoshindwa. Pacquiao, ambaye alistaafu kwa muda mfupi mwaka 2016 na kurejea mwaka huohuo, ameendelea kupanda ulingoni. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 atajaribu kutwaa ubingwa wa welterweight wa Chama cha Ngumi Duniani (WBA) Julai 20 atakapokabiliana na bondia wa Marekani, Keith Thurman, ambaye ni bingwa wa uzito huo na hajawahi kupoteza pambano, wakatapovaana kwenye ukumbi wa MGM Grand.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako