• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa maji Kisarawe kuchochea wawekezaji

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:09:04
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe nchini Tanzania Jokate Mwegelo ameishukuru Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa) kwa kupeleka mradi wa maji katika wilaya ya Kisarawe utakaosaidia kuchochea idadi ya wawekezaji na viwanda. Mwegelo alisema kuwa lengo ni wakazi wa Kisarawe na vitongoji vyake wapate maji ili wawekezaji wajitokeze kwa wingi.

  Amesema mradi huo utasaidia wakazi wa Kisarawe na viunga vyake kupata maji na kutoa nafasi kwa wawekezaji waje kuwekeza kwa wingi kwa sabababu Kisarawe inaendelea kukua kwa kasi hasa kwa sababu inapata maji ya uhakika .

  Mwegelo alisema wawekezaji katika wilaya hiyo wanakabiliwa na changamoto za kukosa maji na umeme na hivyo mradi huo utakapokamilika utaongeza idadi ya wawekezaji wa sekta ya viwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako