• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Safaricom yatoa sababu ya kukawia kuzima nambari za malipo za kampuni za kamari

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:17:14

  Kampuni ya huduma za mawasiliano ya Safaricom imesema itahitaji muda kutekeleza amri ya kuzima nambari za malipo za kampuni za kamari ambazo zilipokonywa leseni za kuhudumu.

  Mawakili wake wameiambia Bodi ya Kudhibiti Michezo ya Kamari Nchni (BCB) kuzima nambari hizo za malipo mara moja kutawasababishia hasara mamilioni wa watumiaji ambao tayari wameweka pesa zao katika kampuni kadha za kamari.

  Safaricom imesema imesema amri hiyo ya bodi hiyo itaathiri zaidi ya wateja 12 milioni.

  Kampuni hiyo ya mawasiliano iliongeza kuwa kampuni mbili za kamari zilikuwa zimepata agizo la mahakama la kuziruhusu kuendelea na shughuli zao bila kuchukua upya leseni za kuhudumu.

  Wakuu wa Safaricom ambao hawakutaka kutajwa majina walisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni sekta ya kamari imekuwa ikiiletea mapato mengi zaidi.

  Kampuni hii hasa huingiza mapato kupitia hudumu za ujumbe mfupi (sms) na M-Pesa.

  Mnamo Jumatano serikali kupitia bodi ya BCB iliziamuru kampuni 27 zilizopigwa marufuku kwa kukoa kitimiza masharti yaliyowekwa, hususan, ulipaji ushuru. Kampuni hizo ni pamoja na sport pesa ,Betin miongoni mwa nyingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako