• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema Marekani inajigamba bila aibu kwa kusema inaweza kutatua masuala yote duniani

  (GMT+08:00) 2019-07-12 20:08:59

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema Marekani inajigamba bila aibu kwa kusema inaweza kutatua masuala yote duniani yakiwemo ya China.

  Bw. Geng ameyasema hayo baada ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence kuwaambia wanahabari kuwa serikali ya Marekani ni kama mnara wa taa ya kuongoza meli ya uhuru duniani, na siku zote inatetea uhuru wa kuabudu duniani, na kwamba mkutano wa "kuhimiza uhuru wa kuabudu" utafanyika mjini Washington wiki ijayo na kujadili masuala husika yanayotokea nchini China na katika sehemu nyingine duniani. Bw. Geng amesema Marekani haina wajibu, idhini ya madaraka na uwezo wa kutatua masuala yote ya dunia, ni bora ishughulikie mambo yake kwanza. Amesisitiza kuwa China inaipinga Marekani kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha dini na kuitaka iangalie kwa usahihi sera za dini na hali ya uhuru wa kuabudu nchini China.

  Wakati huohuo, China imeitaka Canada irekebishe makosa yake na kumwachia huru mara moja ofisa mkuu wa fedha wa kampuni ya Huawei bibi Meng Wanzhou. Habari zinasema waziri wa mambo ya nje wa Canada Bibi Chrystia Freeland hivi karibuni alisema Canada inafuata kanuni ya utawala wa sheria na kumkamata Bibi Meng kwa mujibu wa mkataba wa kubadilishana wahalifu uliopo kati ya Canada na Marekani. Alisema pendekezo lililotolewa na waziri mkuu wa zamani wa Canada Jean Chretien la kumtaka waziri wa sheria kusimamisha kesi ya kumpeleka Bibi Meng Marekani ni kosa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako