• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa ulinzi wa makombora ya S-400 wa Russia wapelekwa Uturuki

  (GMT+08:00) 2019-07-12 20:15:49

  Wizara ya ulinzi wa Uturuki leo imesema shehena ya kwanza ya vifaa vya mfumo wa ulinzi wa makombora ya S-400 wa Russia umesafirishwa leo kwenda Ankara, mji mkuu wa Uturuki.

  Kutokana na mkataba wa ununuzi uliosainiwa kati ya Uturuki na Russia, vifaa hivyo vimeanza kusafirishwa kutoka kwenye kituo cha jeshi la anga cha Murted.

  Ushirikiano kati ya Uturuki na Russia katika mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora umelaaniwa vikali na nchi wanachama wa NATO haswa Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako