• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahitaji ya chakula cha kichina miongoni mwa wakenya yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-07-12 20:21:53
    Mkuu wa chama wa wamiliki wa mahoteli na migahawa wa Kenya Bw. Mike Macharia, amesema mahitaji ya chakula cha kichina miongoni mwa wakenya yameongezeka.

    Bw. Macharia amesema wachina wameleta mambo mapya ya utamaduni wa chakula cha Asia ambao wakenya waliuzoea, na sasa wakenya wameanza kupata ladha mpya. Amesema kwa sasa kama ukienda kwenye mgahawa wa kichina jumapili, utakuwa na bahati kama ukipata nafasi.

    Kenya imekuwa na migahawa ya Kichina tangu ilipopata uhuru mwaka 1963, lakini kumekuwa na ongezeko la migahawa ya Kichina tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Bw. Macharia amesema ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa mapato ya wakenya hasa kupanuka kwa tabaka la kati, na kufanya watafuta chakula mbadala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako