• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wajasiriamali 9,000 wa Afrika watuma maombi kwenye tuzo za Jack Ma za ujasiriamali kwenye mtandao wa Internet

  (GMT+08:00) 2019-07-12 20:22:16

  Zaidi ya wajasiriamali 9,000 wametuma maombi ya tuzo ya mjasiriamali wa mtandao wa internet ya Afrika (ANPI) iliyoanzishwa na Mfuko wa Jack Ma.

  Mkuu wa Kampuni ya Nailab ya Kenya Bw. Sam Gichiru ambayo inashirikiana na mfuko wa Bw. Jack Ma amesema kazi ya kuchagua wajasiriamali wanaostahili tuzo hiyo inafanyika.

  Watu 10 watakaoingia fainali watakuwa na fursa ya kujipatia dola milioni 103 kwenye fainali itakayofanyika mwezi Novemba mbele ya Bw. Jack Ma.

  Kwa mujibu wa waandaaji wa shindano hilo, Bw. Jack Ma yuko tayari kuwaunga mkono wajasiriamali wa Afrika kutokana na kutoa mchango muhimu katika kuleta nafasi za ajira na kupunguza umaskini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako