• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenyekiti wa bunge la Vietnam

  (GMT+08:00) 2019-07-12 20:27:44

  Rais Xi Jinping wa China amekutana na spika wa bunge la Vietnam bibi Nguyen Thi Kim Ngan mjini Beijing.

  Rais Xi amesema, mwaka kesho nchi hizo mbili zitaadhimisha miaka 70 tangu zianzishe uhusiano wa kidiplomasia. Nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia hali ya ujumla, kuhimiza urafiki na kuongeza ushirikiano ili kusukuma mbele uhusiano wa pande hizo mbili. Pia rais Xi amesifu ushirikiano kati ya bunge la umma la China na bunge la Vietnam, na kutarajia pande hizo mbili zichukue hatua zaidi kuongeza maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi wa kuimarisha msingi wa maoni ya umma wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

  Kwa upande wake bibi Nguyen Thi Kim Ngan amesema, Vietnam inatarajia kushirikiana na China kuendelea kuungana mkono katika njia ya maendeleo ya Kijamii, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, na kudhibiti tofauti zilizopo ili kusukuma mbele wenzi wa kimkakati kati yao upate maendeleo zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako