• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu zafikia makubaliano kuhusu kulinda haki za wafanyakazi

    (GMT+08:00) 2019-07-13 17:19:56

    Uganda na Umoja wa Falme za kiarabu zimesaini makubaliano yatakayosaidia kulinda maslahi ya wafanyakazi wa Uganda nchini Falme za kiarabu.

    Waziri wa jinsia, nguvu kazi na maendeleo ya jamii wa Uganda Bibi Janat Mukwaya, amesema makubaliano hayo yalifikiwa Juni 26, yakiwa na lengo la kulinda haki za wafanyakazi wahamiaji wa Uganda nchini Falme za Kiarabu. Bibi Mukwaya amesema baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, mazingira ya wafanyakazi waganda nchini Falme za Kiarabu yatazingatia makubaliano hayo kabla ya wafanyakazi waganda hawajaondoka Uganda.

    Pia amesema baada ya kusaini makubaliano hayo, Umoja wa Falme za Kiarabu imeomba wafanyakazi elfu 80 kutoka Uganda katika kipindi cha miaka 12 ijayo. Bibi Mukwaya pia imesema Uganda imesaini makubaliano kama hayo na Jordan na Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako