• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo nchini Sudan yaahirishwa

    (GMT+08:00) 2019-07-14 17:52:16

    Mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Sudan Bw. Mohamed Hacen Lebatt ametangaza kwamba mazungumzo kati ya Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan (TMC) na wapinzani Muungano wa Uhuru na Mabadiliko yameahirishwa hadi Jumapili kutokana na ombi la upande wa upinzani la kupata ushauri zaidi.

    Siku ya Ijumaa, TMC na Muungano wa upinzani walikubaliana juu ya tamko la kisiasa, ambalo linaamua mamlaka yote ya kipindi cha mpito. Awali tarehe 5 Julai, pande hizo mbili zilikubaliana kuanzishwa kwa serikali ya kiraia na baraza la mamlaka la pamoja la miaka mitatu ambalo litaongozwa na maofisa na wanajeshi kwa zamu, na pia zilikubaliana kuchelewesha uanzishwaji wa baraza la kisheria mpaka lianzishwe baraza huru na serikali ya kiraia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako