• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa aadhimisha Siku ya Taifa hilo kwa kuzingatia zaidi operesheni za ulinzi wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-07-15 08:36:48

    Ufaransa imeadhimisha Siku ya Taifa hilo hapo jana kwa kufanyika kwa gwaride la jeshi katika mtaa maarufu wa Champs Elysees mjini Paris.

    Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo aliwakaribisha viongozi kutoka nchi wanachama wa Pendekezo la Mwingiliano wa Ulaya (E21), ikiwemo Ujerumani, Uholanzi, Uingereza, Hispania na Denmark, na kuwataka kuchukua hatua za haraka kuunda kikosi cha dharura cha Ulaya kitakacholinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo.

    Rais Macron amesema, kuanzishwa kwa kikosi hicho ni kipaumbele kwa Ufaransa, na kwamba kufanya kazi kwa pamoja na kuimarisha uwezo wa nchi hizo wa kuchukua hatua kwa pamoja ni changamoto kwa Pendekezo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako