• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanadiplomasia wa Uingereza asema Trump amejiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran kumpinga Obama

    (GMT+08:00) 2019-07-15 08:37:10

    Gazeti la Daily Mail la Uingereza limenukuu ujumbe uliovuja unaodai kuwa, rais Donald Trump wa Marekani ameitoa nchi hiyo kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran kwa lengo la kumkera mtangulizi wake, Barack Obama.

    Ujumbe huo ulioandikwa na aliyekuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch, umesema uamuzi wa kujitoa kwenye makubaliano hayo ni uhalifu wa kidiplomasia, ambao una malengo ya kibinafsi. Pia katika ujumbe huo, Darroch aliandika kuwa kuna mgawanyiko kati ya washauri wa rais Trump, na kwamba ikulu ya Marekani inakosa mkakati wa mambo ya kufanya baada ya kujitoa kwenye makubaliano hayo.

    Uingereza imeanza uchunguzi ili kufahamu mtu aliyevujisha taarifa hizo, na habari zinasema tayari mtuhumiwa amekamatwa na tukio hilo linahusiana na udukuzi wa kampyuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako