• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TWENZETU AFCON 2019: Nyama sasa zimeanza kuonekana kwenye mtori, Senegal, Algeria zatinga fainali

  (GMT+08:00) 2019-07-15 09:38:18

  Ni Algeria dhidi ya Senegal kwenye fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2019.

  Timu hizo ambazo zilianza mashindano katika kundi C na Tanzania na Kenya zimeibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao na kukata tiketi ya kumenyana tena kwenye fainali.

  Goli la kujifunga la Tunisia katika muda wa nyongeza limewavusha Senegal mpaka hatua ya fainali Japo wengi waliipigia debe Senegal kushinda mchezo huo, lakini ushindi haukuwa rahisi, Tunisia wamepambana.

  Nusu fainali ya pili baina ya Algeria na Nigeria ilitimua vumbi majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki9, jijini Cairo. Ndoto za Nigeria kuchukua kombe hilo kwa mara ya nne zimezimwa kwa kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa mbweha wa jangwani, Algeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako