• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la taifa la China laongezeka kwa asilimia 6.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka

    (GMT+08:00) 2019-07-15 18:15:46

    Takwimu mpya zinazotolewa na idara ya takwimu ya taifa ya China zimeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la taifa la China GDP limeongezeka kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwaka jana. Msemaji wa idara hiyo Bw. Mao Shengyong amesema, pande tatu za matumizi, uwekezaji na mauzo ya bidhaa kwa nje na uagizaji wa bidhaa kutoka nje zinaendelea kwa utulivu, na uchumi wa China unaendelea kwa utulivu katika nusu ya kwanza ya mwaka.

    Kwa mujibu wa takwimu hizo mpya, katika nusu ya kwanza ya mwaka pato la taifa la China limezidi dola trilioni 6.5 za kimarekani, ambayo imeongezeka kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na ya mwaka jana. Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bw. Mao Shengyong amesema, ongezeko hilo lenye sifa ya juu sio kazi rahisi.

    "Wakati tukizungumzia ongezeko la asilimia 6.3 la uchumi, tunatakiwa kufahamu kuwa hali ya soko la ajira ina utulivu, gharama za maisha zinadumisha mwelekeo wa kuongezeka kwa kiasi kidogo au kutulia, na mapato ya wakazi yanaongezeka kwa kasi. Wakati huohuo, tunapaswa kuona matumizi ya nishati kwa GDP ya dola 1,455 za kimarekani yanapungua kwa asilimia 2.7, ambayo yanamaanisha kuwa mazingira ya kiikolojia yanaboreshwa. Hivyo ongezeko hilo la asilimia 6.3 ni ongezeko lenye sifa ya juu na uendelevu".

    Ofisa huyo amesema, tangu mwaka jana kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia, ikiwemo kufufuka kwa uchumi wa dunia inapungua, migongano ya utaratibu inayoongezeka nchini China inaonekana zaidi, na uchumi wa China unakabiliwa na shinikizo la kupungua. Bw. Mao anasema,

    "Katika hali hiyo, hatukuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi, bali tumehimiza mageuzi na uvumbuzi nchini. Tunachochea uhalali wa soko, kuhimiza uchumi kukua kwa utulivu kupitia uvumbuzi na uratibu, kuboresha mazingira ya kibiashara na kupunguza kwa kiasi kikubwa ushuru na gharama za matumizi."

    Takwimu zinaonesha kuwa tangu mwezi Januari hadi Juni mwaka huu, thamani ya ziada ya sekta ya viwanda imeongezeka kwa asilimia 6, huku sekta ya utoaji wa huduma pia ikiongezeka kwa kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako