• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtu wa kwanza athibitishwa kuambukizwa homa ya Ebola masharikki mwa mji wa Goma, DRC

    (GMT+08:00) 2019-07-15 18:45:28

    Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imesema mtu wa kwanza amethibitishwa kuambukizwa homa ya Ebola mjini Goma, mashariki mwa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema mchungaji mmoja aliyewahi kuathiriwa na maambukizi ya homa ya Ebola mjini Butembo, kaskazini mashariki mwa DRC, alikuwa mgonjwa wiki iliyopita, na kuelekea mjini Goma kwa basi. Baadaye mtu huyo alithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo na kupelekwa kupatiwa matibabu.

    Raundi ya kumi ya homa ya Ebola imesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,600 nchini DRC. Tawi la madaktari kutoka kikundi cha 22 cha walinzi wa amani wa China nchini DRC, limeimarisha tathmini juu ya hali ya hatari ya ugonjwa huo. Hadi sasa hakuna mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo katika eneo la opresheni zake lililoko Bukavu mkoani Kivu Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako