• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabalozi wa nchi 37 waunga mkono msimamo wa China kuhusu Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-07-15 19:36:18

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amezungumzia tukio kwamba mabalozi wa nchi 37 wameandika barua kwa pamoja kwa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono msimamo wa China kuhusu suala la Xinjiang, huku akisisitiza kuwa barua hiyo ni jibu lenye nguvu kwa shutuma zisizo na msingi dhidi ya China kutoka baadhi ya nchi za magharibi.

    Barua hiyo iliyoandikiwa na mabalozi wa kudumu wa nchi 37 mjini Geneva imeyapongeza mafanikio ya China katika kuendeleza shughuli za haki za binadamu za Xinjiang, kupambana na ugaidi na kuondoa msimamo mkali, huku ikisifu China kwa kuwaalika mabalozi wa nchi mbalimbali, maofisa wa mashirika ya kimataifa na waandishi wa habari kutembelea Xinjiang. Mabalozi hao pia wamehimiza nchi kadhaa kutoilaumu China bila sababu kupitia habari zisizothibitishwa. Aidha, Bw. Geng amesifu na kushukuru nchi hizo kutoa maoni ya wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako