• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mashabiki wa Arsenal wamcharukia mmiliki wa klabu

    (GMT+08:00) 2019-07-16 07:58:42
    Mashabiki wa washika bunduki wa London –Arsenal wamechoshwa na vitendo vya mmiliki mwenye hisa nyingi za klabu hiyo, Stan Kroenke vinavyoifanya iporomoke na wamemuandikia waraka wakitaka aanze kuchukua hatua kuihuisha ili iwe na nguvu mpya.

    Makundi makubwa ya mashabiki wa Arsenal yameungana na kutoa taarifa hiyo kwa tajiri huyo raia wa Marekani. Arsenal inajiandaa kushiriki michuano ya EUROPA kwa mara ya tatu mfuluilizo baada ya kushindwa kumaliza msimu uliopita wa ligi kuu ya Uingereza katika nafasi ya nne. Hadi sasa klabu hiyo toka kaskazini mwa jiji la London imenunua mchezaji mmoja tu ambaye ni kinda Mbrazili Gabriel Matinelli akiwa ni mchezaji pekee mpya katika kikosi cha Unai Emery.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako