• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Houthi wa Yemen washambulia uwanja wa ndege wa jeshi la Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:05:59

    Waasi wa Houthi wa Yemen wamesema wamefanya mashambulizi makubwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya uwanja wa ndege wa jeshi wa Mfalme Khaled, kusini mwa Saudi Arabia.

    Kituo cha televisheni cha kundi hilo al-Masirah kimeripoti kuwa, mashambulizi hayo yalifanyika jana saa moja baada ya mazungumzo ya amani ya siku mbili chini ya Umoja wa Mataifa kati ya wawakilishi wa kundi la Houthi linaloungwa mkono na Iran na serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudia iliyoko uhamishoni.

    Msemaji wa kundi hilo Yahya Sarea amesema, mashambulizi hayo ni majibu ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen.

    Serikali ya Saudi Arabia haijatoa kauli yoyote kuhusu shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako