• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa UM asema huduma za fedha kidijitali zinaweza kusaidia Afrika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:06:07

    Ofisa wa Umoja wa Mataifa amesema huduma za fedha kidijitali zinaweza kuisaidia Afrika kuharakisha kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja huo.

    Mkurugenzi wa sekretarieti ya kikosi kazi kinachoshughulika na huduma za fedha kidijitali za malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyo chini ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Tillman Bruett amesema hayo kando ya ufunguzi wa tamasha la teknolojia na huduma za fedha kati ya Afrika na Asia. Bw. Bruett ameliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa, huduma za fedha kidijitali zimetoa fursa kwa familia kutimiza malengo yao ya maendeleo endelevu kwa kuwawezesha kulipa na kupata huduma za matibabu ya afya na nishati safi.

    Habari zinasema, tamasha hilo la siku mbili limewakutanisha watunga sera na wataalam wa mambo ya fedha zaidi ya 1,500 kutoka nchi 45 za Asia na Afrika na linalenga kuhimiza matumizi ya teknolojia na huduma za fedha katika kanda hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako