• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yapata dola za Marekani milioni 100 kuendeleza uvumbuzi na teknolojia

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:06:33

    Ethiopia na Nchi za Kifalme za Kiarabu UAE zimesaini makubaliano yenye thamani ya dola za Marekani milioni 100 yanayolenga kuunga mkono juhudi za serikali ya Ethiopia katika sekta za uvumbuzi na teknolojia.

    Waziri wa uvumbuzi na teknolojia wa Ethiopia Getahun Mekuria amesema, fedha hizo zitakazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Makampuni wa Khalifa, zitasaidia makampuni ya kilimo, usindikaji wa bidhaa za kilimo, habari, huduma za teknolojia, nishati na utengenezaji.

    Habari zinasema, waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed amehimiza vijana wa Ethiopia kujitahidi katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ili kutoa mchango katika maendeleo ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako