• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wapongeza Kongamano la Amani na Usalama kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:10:28

    Umoja wa Afrika umepongeza Kongamano la kwanza la Amani na Usalama kati ya China na Afrika linalofanyika mjini Beijing kwa kuhimiza utulivu barani Afrika.

    Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Umoja huo anayeshughulikia mambo ya amani na usalama Bw. Smail Chergui ambaye amesisitiza umuhimu wa kongamano hilo katika kuhimiza ushirikiano kati ya Afrika na China katika juhudi za kujenga amani barani Afrika.

    Amesema kongamano hilo limefanyika wakati Afrika inakabiliwa na ukosefu wa usalama na kujitahidi kukomesha migogoro yote katika bara hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako