• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO, OCHA waitisha mkutano kutokana na maambukizi mapya ya Ebola nchini DRC

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:40:42

    Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imethibitisha kuwa, mtu mmoja amethibitishwa kuwa na maambukizi ya homa ya Ebola mjini Goma, mashariki mwa nchi hiyo. Mtu huyo aliyetokea Butembo, kaskazini mashariki mwa DRC, alikuwa mgonjwa wiki iliyopita, na kuelekea mjini Goma kwa basi. Jumuiya ya kimataifa na nchi jirani zimechukua tahadhari kutokana na maambukizi hayo mapya.

    Shirika la Afya Duniani WHO na ofisi ya kuratibu mambo ya binadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA jana zilisema mkutano wa ngazi ya juu kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC umeahidi kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na serikali ya nchi hiyo na mbinu ya mfumo mpana ya Umoja wa Mataifa.

    Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, kwa kushirikiana na serikali, inawezekana kutokomeza maambukizi hayo. Amesema pande hizo mbili zina vifaa bora zaidi vya afya ya umma kukabiliana na Ebola, ikiwemo chanjo zenye ufanisi.

    Taarifa iliyotolewa kwenye mkutano huo inasema, maambukizi ya Ebola bado yamedhibitiwa ndani ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, lakini njia za kukabiliana nayo ziko kwenye kipindi muhimu. WHO imefanya tathimini ya hatari ya kuenea kwa virusi vya homa hiyo katika mikoa jirani na nchi jirani.

    Wakati huohuo, wafanyakazi wawili wa Afya wanaoshughukilia ugonjwa wa Ebola wameuawa wikiendi iliyopita kaskazini mwa DRC. Wizara ya afya ya nchi hiyo imesema, wafanyakazi hao waliuawa nyumbani kwao katika jimbo la Kivu Kaskazini baada ya kutishiwa kwa miezi kadhaa.

    Bw. Tedros amesema, inapaswa kutokomeza mashambulizi na maingiliano mengine dhidi ya juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo. Pia juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono kisiasa kutoka pande zote, mashirika ya kijamii, ili kufanya kazi kwa usalama na bila ya kuingiliwa, kwani hiyo ndio pekee ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

    Nchini Burundi, Wizara ya afya jana ilisema, itatoa chanjo kwa wahudumu wa afya na maofisa wa uhamiaji katika eneo la mpaka ili kukabiliana na Ebola. Chanjo hizo zitawasili Burundi leo.

    Nchi jirani ya Rwanda nayo imetoa onyo kwa wananchi wake kutofanya safari zisizo za lazima kwenda Goma, DRC. Onyo hilo limetolewa na wizara ya afya ya Rwanda wakati kila siku watu karibu laki 1 wanasafiri kati ya mji wa Goma na eneo la Rubavu, Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako