• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande hasimu nchini Sudan Kusini zahimizwa kutekeleza makubaliano ya amani ili kupunguza njaa

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:06:46

    Wataalam wamehimiza pande zinazopambana nchini Sudan Kusini kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya amani ili kupunguza viwango vya juu vya njaa katika nchi hiyo ambayo imeshuhudia wakimbizi wa ndani kutokana na mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka mitano.

    Mtafiti wa Mfuko wa Amani Duniani WPF Bw. Tong Deng Anei amesema, hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini bado ni mbaya ambapo maelfu ya watu katika majimbo ya Unity, Bahr el Ghazal Kaskazini na Yei wanakabiliwa na hatari kubwa ya njaa baada ya kushindwa kupata chakula na kufungwa kwa masoko kutokana na mapigano.

    Bw. Anei pia amelaumu kufungwa kwa muda mrefu kwa mpaka wa nchi hiyo na Sudan ambao umesababisha uhaba wa chakula katika majimbo ya Bahr el Ghazal Kaskazini na Warrap.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako