• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko tulivu la uchumi wa China linanufaisha uchumi wa Marekani na dunia

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:19:09

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, ongezeko tulivu la uchumi wa China linanufaisha uchumi wa dunia na wa Marekani pia.

    Bw. Geng Shuang amesema, licha ya kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia na kuongezeka kwa sintofahamu na hali ya kukosekana utulivu, pato la taifa la China GDP lilikua kwa asilimia 6.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kiwango ambacho ni kizuri kuliko makundi mengi ya uchumi duniani.

    Bw. Geng Shuang amesema, kauli ya Marekani kuwa "China inajitahidi kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani kutokana na kasi ya uchumi wake kupungua" haina ukweli wowote. Amesema jambo hilo si matarajio ya China peke yake, Marekani pia ina mahitaji hiyo. Watu wa nyanja mbalimbali na wateja wengi nchini Marekani, pia wanapinga kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China na vita vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako