• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yatoa wito wa juhudi za pamoja katika kusaidia wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:23:04

    Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeitaka jamii ya kimataifa na wenzi wake wa kibinadamu kuongeza juhudi za pamoja ili kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia.

    WFP ilitoa wito huo jana wakati ikipokea tani elfu 16 za mchele zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 13 kutoka kwa serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia.

    Mkurugenzi wa Shirika hilo nchini Ethiopia Bw. Steven Were Omamo amesema, msaada hio umekuja katika wakati muhimu ambapo shirika hilo linakabiliwa na uhaba wa fedha za kuendeleza shughuli zake za kibinadamu nchini Ethiopia, hususan kwa wakimbizi na wakimbizi wa ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako