• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya huduma za kifedha mtandaoni ya Afrika kuimarisha huduma za malipo za Wechat na Alipay

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:41:11

    Kampuni ya malipo ya Wapi Pay ya Afrika imesema, inapanga kuharakisha kutumia huduma za malipo za Wechat na Alipay barani Afrika, ili kuhimiza biashara kati ya China na Afrika.

    Mkuu mtendaji wa Wapi Pay Bw. Paul Ndichu ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, kampuni yake inatoa huduma za malipo katika nchi 7 za Afrika, na inapanga kuunganisha nchi 24 za Afrika na China katika miaka miwili ijayo, ili kutoa huduma ya kusafirisha pesa mtandaoni kati ya pande hizo.

    Amesema kutokana na teknolojia za huduma za kifedha ya kampuni hiyo, muda wa kusafirisha pesa kati ya Afrika na China umepungua na kuwa sekunde 30 tu, badala ya zaidi ya siku tatu kati ya benki na benki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako