• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito nchi zote kujiendeleza kwa njia ya haki na shirikishi

    (GMT+08:00) 2019-07-17 19:17:29

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kuwa nchi zote zinatakiwa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kwa njia ya haki na shirikishi.

    Bw. Guterres amesema hayo kwenye mkutano wa mawaziri wa baraza la kisiasa la juu la maendeleo endelevu la mwaka 2030, akiongeza kuwa kutokana na juhudi za miaka kadhaa, utekelezaji ya malengo hayo bado haujakamilika kama ulivyopangwa, na hali ya dunia bado si nzuri. Aidha akizungumza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ametoa wito kwa nchi husika kuchangia fedha kwenye Mfuko wa hali ya hewa.

    Baraza hilo linafanyika mara moja kwa mwaka, na baraza la mwaka huu limefanyika tarehe 9 hadi 18 mjini New York, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Ajenda kuu ni "kuwapatia watu haki na uwezo, na kuhakikisha haki na usawa". Kwenye baraza hilo, nchi karibu 50 zimekabidhi taarifa ya nchi ya hiari, zikitathmini kwa pamoja hali ya utekelezaji wa malengo ya elimu, ajira, kupunguza hali ya kutokuwa na usawa, na kuchukua hatua za kuboresha hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako