• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wawakilishi wa Afrika wasifu umuhimu wa kiujenzi wa China katika sekta ya amani na usalama

  (GMT+08:00) 2019-07-17 19:56:45

  Mkutano wa kwanza wa amani na usalama kati ya China na Afrika umefunguliwa tarehe 15 mjini Beijing, na kuhudhuriwa na mawaziri wa ulinzi na wanadhimu wakuu 15 wa majeshi kutoka nchi za Afrika zikiwemo Cameroon na Ghana, wajumbe waandamizi wa nchi 50 za Afrika na idara za ulinzi za Umoja wa Afrika, pamoja na wawakilishi wa jeshi la China. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe kutoka Afrika wamesifu mchango wa kiujenzi uliotolewa na China katika sekta ya amani na usalama.

  Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, kamishna wa amani na usalama ya Umoja wa Afrika Bw. Smail Chergui amesema, uhusiano wa kiwenzi na kimkakati na China umechangia kuimarisha kazi ya Umoja huo katika kulinda amani na usalama barani Afrika. Bw. Chergui anasema:

  "Ahadi alizotoa rais Xi Jinping wa China wakati wa Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana, zimetusaidia kutafuta ufumbuzi wa masuala ya amani na usalama yanayokabili eneo la Sahel, ukanda wa Ziwa Chad na Pembe ya Afrika. Ningependa kutumia fursa hii leo kutoa shukrani kwa China kutokana na uungaji mkono wake wa kudumu kwa Umoja wa Afrika katika kuhimiza amani na usalama barani Afrika."

  Mkuu wa idara ya rasilimali ya watu katika Wizara ya Ulinzi ya Tanzania Bw. Blasius Kalima Masanja amepongeza umuhimu wa kiujenzi wa China katika kuhimiza bara la Afrika kutimiza usalama wa pamoja, wenye ushirikiano na wa kudumu, na kusisitiza kwamba kukabiliana na tishio la usalama barani Afrika kunahitaji ushiriki wa pande zote ikiwemo China. Bw. Masanja anasema:

  "Tunahitaji kujadili namna ya kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika katika amani na usalama upande na kufikia kiwango kipya. Kukabiliana na tishio la usalama kwa Afrika kunahitaji juhudi za pamoja zikiwemo nchi na kanda mbalimbali, haswa unahitaji urafiki wetu na China."

  Mkutano wa kwanza wa Baraza la amani na usalama kati ya China na Afrika umeandaliwa na Wizara ya ulinzi ya China, kauli mbiu yake ni "Kujenga usalama kwa ushirikiano", na utamalizika tarehe 20 mwezi huu. Washiriki wa mkutano huo watajadili na kutafiti mapendekezo muhimu kuhusu "kujenga usalama kwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika kwa ushirikiano", ambayo yalitolewa kwenye Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2018. Wakati wa mkutano huo, wajumbe wa Afrika watatembea majeshi ya nchi kavu, majini na angani ya China na mji wa Shanghai.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako