• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TWENZETU AFCON 2019: Mechi ya kusaka mshindi wa tatu imechezwa jana, ni Super Eagles ndio mshindi

  (GMT+08:00) 2019-07-18 09:24:58

  Baada ya kuchezeshwa mchakamchaka wiki iliyopita kwenye hatua ya nusu fainali, jana zimekutana katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika yanayofikia ukiongoni nchini Misri.

  Super Eagles ya Nigeria imefanikiwa kukamata nafasi ya tatu na kuondoka na medali ya shaba baada ya kuifunga Tunisia kwa goli 1-0. Goli lililopachikwa kimiani na Odion Ighalo dakika ya 3 ya mchezo.

  Kesho ndio kesho, mafahari wawili, Mbweha wa jangwani Algeria itakapovaana na Simba wa Teranga ya Senegal katika mchezo wa fainali na kuhitimisha mashindano hayo. Ni nani atachukua ubingwa wa Afrika?majibu tutayapata ama baada ya dakika 90, ama dakika 120, am ahata kwa njia ya matuta, lakini kesho lazima kieleweke.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako