• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-'Uchumi wa Kadogo' waongoza sekta ya rejareja

    (GMT+08:00) 2019-07-19 07:49:58

    Zaidi ya asilimia 70 ya bidhaa zinazouzwa kwa wingi nchini Kenya ni bidhaa zinazogharimu chini ya Sh55,hii ikiashiria kwamba soko lisilo rasmi nchini Kenya maarufu "uchumi wa kadogo" bado ndio unaoongoza nchini humu.

    Hii ni kwa mujibu wa wa utafiti masoko wa shiriki la Nielsen ambapo,kwenye Ripoti ambayo shirika hilo iliitoa jana inaonyesha kuwa biashara ya zamani kwenye vibanda maarufu vioski ndio kunakofanyika miamala mingi ya rejareja.

    Ripoti hiyo inasema kuwa miamala mingi katika sekta ya rejareja ni chini ya dola 1 (Sh103) nah ii inaashiria ukuaji wa sekta ya rejareja katika biashara manunuzi madogo.

    Manunuzi madogo,kulingana na Ripoti ya Nielsen yameandikisha asilimia 66.3 ya jumla ya matumizi katika robo ya kwanz aya mwaka 2019,ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.7 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako