• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano kati ya TMC na kundi la upinzani la Sudan waahirishwa

    (GMT+08:00) 2019-07-19 09:19:33

    Mkuu wa Muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko nchini Sudan Bw. Munzir Abul-Mali amesema, mkutano kati ya muungano huo na Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan, TMC kuhusu azimio la kikatiba uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa kwa muda usiojulikana. Hata hivyo, hakutoa sababu za kuahirishwa tena kwa mkutano.

    Jumatano wiki hii, pande hizo mbili zilisaini muswada wa azimio hilo la kisiasa, ikiwa ni hatua ya kufikia makubaliano na kujenga mfumo wa kipindi cha mpito.

    Pande hizo mbili pia zilikubaliana kuahirisha kusainiwa kwa azimio la kikatiba, ambalo linaelekeza utaratibu wa mgawanyo wa madaraka katika kipindi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako