• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: TWENZETU AFCON 2019: Leo ndio leo, nyasi zitawaka moto, makocha wazawa kukutana katika fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 21

  (GMT+08:00) 2019-07-19 09:26:31

  Fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2019) inayofikia kilele leo nchini Misri baina ya Algeria na Senegal, itawakutanisha makocha wazawa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21,

  Kocha wa mbweha wa jangwani Algeria Djamel Belmadi na Kocha wa Simba wa Teranga ya Senegal Aliou Cisse wote walikuwa wachezaji wa kiungo na waliwahi kuchezea klabu za Uingereza katika ligi kuu ya EPL.

  Mara ya mwisho kukutanisha makocha wazawa ilikuwa mwaka 1998 wakati Misri iliyokuwa ikifundishwa na kocha Mahmoud el Gohary ilikutana na Afrika Kusini iliyokuwa chini ya kocha Ephraim Sono.

  Waswahili wanasema mtoto hatumwi dukani leo, nani kuibuka na ubingwa? Wadau wa soka wamegawanyika wengine wanarusha karata yao kwa Senegal wengine kwa Algeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako