• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MPIRA WA PETE: New Zealand yaizidi Australia kwa goli moja na kutwaa kombe la dunia la mpira wa pete

  (GMT+08:00) 2019-07-22 14:10:17

  New Zealand jana iliwashika pabaya mabingwa wa mara 11 wa mpira wa pete wa kombe la dunia Australia na kuondoka na taji huko Liverpool. Fainali zilikuwa za pata shika nguo kuchanika mwanzo hadi mwisho na katika dakika za majeruhi New Zealand ikaizidi Australia kwa goli 1 na kuwa wababe wa mwaka huu ambapo matokeo yalikuwa 52-51. Ni taji la tano hili kwa New Zealand lakini ni la kwanza tangu walipomaliza utawala wao mwaka 2003. Uingereza imeondoka wakiwa nafasi ya tatu kwa kuchukua shaba baada ya kuwachakaza Afrika Kusini kwa magoli 58-42 katika mechi yao ya kutafuta mshindi wa tatu iliyochezwa mapema jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako