• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China azungumza na mrithi wa ufalme wa Abu Dhabi wa Falme za Kiarabu

  (GMT+08:00) 2019-07-22 16:45:29

  Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mrithi wa ufalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan ambaye yupo ziarani nchini China. Rais Xi amesema, uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zenye utamaduni na mtindo tofauti na kutoka kwenye kanda tofauti, na China inapenda kushirikiana na Falme za Kiarabu kuhimiza uhusiano huo kupata mafanikio mapya, ili kuwanufaisha wananchi wao.

  Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesema China inaichukulia Falme za Kiarabu kama mwenzi muhimu wa ushirikiano wa kimkakati katika sehemu ya Mashariki ya Kati, na kuiunga nchi hiyo kufanya kazi kubwa zaidi katika mambo ya kikanda na kimataifa. Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kukuza maelewano ya kisiasa na mawasiliano ya kimkakati, na kuharakisha ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema,

  "Katika ziara yako, tutatoa taarifa ya pamoja ya kuimarisha zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Falme za Kiarabu, ambayo itakuwa taarifa nyingine muhimu katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizi. Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na pia ni mwaka wa 35 tangu nchi zetu zianzishe uhusiano wa kibalozi. Napenda kushirikiana nawe kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi zetu kupata mafanikio mapya, ili kuwanufaisha zaidi wananchi wetu."

  Rais Xi amesisitiza kuwa amani na utuliuvu kwenye sehemu ya Ghuba ni muhimu sana kwa usalama na maendeleo ya Mashariki ya Kati na hata dunia nzima, sehemu hiyo inatakiwa kuendelea kuwa "sehemu ya usalama" badala ya "chanzo cha msukosuko". Ameongeza kuwa China inaiunga mkono Falme za Kiarabu kwa kujitahidi kulinda amani na utulivu wa kikanda, na kupenda kushirikiana na nchi hiyo pamoja na jumuiya ya kimataifa kutoa mchango kwa ajili ya kuhakikisha amani na utulivu wa sehemu ya Ghuba.

  Sheikh Mohammed amesema, Falme za Kiarabu inaona kuwa maendeleo ya China yana mustakabali mzuri, na bila kujali mabadiliko ya hali ya dunia, nchi hiyo itakuwa mwezi mzuri zaidi wa ushirikiano wa kimkakati wa China. Akisema,

  "Tunaona fahari kubwa kwamba mwaka jana ulifanya ziara ya kihistoria nchini Falme za Kiarabu. Katika ziara hiyo, tuliinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi zetu kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote, na huu ni uthibitisho wa maingiliano imara kati ya serikali zetu na wananchi wetu."

  Sheikh Mohammed amesema, Falme za Kiarabu inaipongeza China kwa juhudi za kulinda maslahi ya watu wa makabila madogo, na kuhimiza mshikamano na masikilizano kati ya makabila tofauti, na kupenda kushirikiana na China katika mapambano dhidi ya ugaidi, ikiwemo kundi la Tukistan ya Mashariki, ili kulinda usalama wa kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako