• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa bomu Somalia yaongezeka hadi 17

  (GMT+08:00) 2019-07-23 08:31:22

  Maofisa afya nchini Somalia wamethibitisha kuwa, idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari huko Mogadishu, imeongezeka na kufikia 17, na watu wengine 28 kujeruhiwa.

  Mkurugenzi wa Hospitali ya Medina Bw. Mohamed Yusuf amesema, watu 12 kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

  Polisi imesema gari lililotegwa mabomu lililipuka katika kituo cha ukaguzi wa usalama kilichoko kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde huko Mogadishu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako