• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu mpya wa Uingereza akaribia kutangazwa

    (GMT+08:00) 2019-07-23 08:47:58

    Zoezi la kuhesabu kura limeanza jana usiku nchini Uingereza ambalo litaamua nani atakuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

    Upigaji kura kwa wanachama wa Chama cha Conservatives ulimalizika jana saa 11 jioni kwa saa za huko, ikiwa ni saa chache baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Sir Alan Duncan kujiuzulu wadhifa wake akipinga dhidi ya uwezekano wa Boris Johnson kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

    Mawaziri wengine, akiwemo waziri wa fedha Philip Hammond na waziri wa sheria David Gauke wamesema wazi kuwa watajiuzulu nyadhifa zao kama Bw. Johnson atatangazwa kuwa mshindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako