• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KASHFA- Ronaldo kutokabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono

  (GMT+08:00) 2019-07-23 14:03:56

  Waendesha mashtaka wa Marekani wamesema nyota wa soka Cristiano Ronaldo hatakabiliwa na shitaka lolote baada ya kutuhumiwa kuhusika na unyanyasaji wa kingono. Tuhuma hizo zilitolewa na Kathryn Mayorga, 34, aliyedai kuwa mchezaji huyo wa klabu ya Juventus alimbaka katika hoteli moja mjini Las Vegas mwaka 2009. Iliripotiwa kuwa Bi Mayorga alikubaliana na nyota huyo kusuluhisha kesi hiyo kimya kimya nje ya mahakama mwaka 2010. Lakini aliamua kufungua tena kesi hiyo mwaka 2018, baada ya Ronaldo kupinga madai hayo. Katika taarifa iliyotolewa jana Jumatatu, waendesha mashitaka wa Las Vegas walisema madai hayo hayakuweza kuthibitishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako