• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahandisi wa Uganda waomba kupewa taarifa kuhusu kandarasi kwenye sekta ya petrol na mafuta

    (GMT+08:00) 2019-07-24 19:17:00

    Wahandisi wa ujenzi nchini Uganda wamezitaka kampuni za mafuta kuwapa maelezo kikamilifu kuhusu kandarasi wanazotoa. Mwakilishi wa chama cha wahandisi nchini Uganda Bwana Moses Kaitaka amesema iwapo hawatakuwa na maelezo ya kutosha huenda wakakosa fursa za kupata kazi kwenye sekta hiyo.Kaitaka amezitaka kampuni hizo kuhakikisha taarifa zote za kila mwaka za manunuzi zinatolewa kwa wakati ili wapate fursa kama wengine.Kitaka alisema hayo wakati wa kongamano la kujadili fursa zilizopo kwenye sekta ya mafuta na gesi lililoandaliwa na na mamlaka ya mafuta nchini Uganda katika jiji la Kampala.Kongamano hilo lilikuwa linalenga kuandaa kampuni kwa awamu ya kwanza ya maendeleo ya gesi na mafuta kwa mipango ya ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta nchini humo.Katibu wa kudumu katika wizara ya nishati na madini wa Uganda Bw Robert Kisande amezitaka kampuni zote nchini humo kufuata maagizo yanayotakiwa wakati wa utoahi tenda au wanyimwe nafasi za kufurahia fursa zilizopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako