• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rotich na Thugge wakanusha mashtaka ya ufujaji fedha

    (GMT+08:00) 2019-07-24 19:17:26

    Waziri wa Fedha wa Kenya Henry Rotich na katibu wake Thugge Kamau wamekanusha mashtaka ya ufujaji fedha za mabwawa mawili. wawili hao na maafisa wengine wanasemekana kushirikiana kufuja shilingi bilioni 17. Rotich, Thugge na maafisa wengine wakuu serikalini walikaa kimya kizimbani wakati wakisomewa mashtaka ya kuongeza thamani ya ujenzi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer kwa shilingi bilioni 17 katika mahakama ya Milimani.

    Licha ya wizara ya fedha kutoa kima cha shilingi milioni sita, kwa ununuzi wa kipande cha ardhi, kiongozi wa mashtaka alisema kuwa hakuna kipande chochote chaa ardhi kilichonunuliwa. Aidha maafisa hao wakuu katika wizara ya fedha walishtakiwa kwa makosa ya ufisadi, matumizi mabaya ya afisi, matumizi mabaya ya fedha na pia njama za kuiba shilingi bilioni 17. Kwa sasa wizara ya fedha haina uongozi kwani waziri na katibu wake wanakabiliwa na makosa ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako