• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu mpya wa Uingereza aunda timu ya juu katika mabadiliko makubwa kwa zaidi ya miaka 50

    (GMT+08:00) 2019-07-25 09:13:01

    Waziri mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson ameteua mawaziri wa awamu ya mwanzo jana usiku, saa chache baada ya kushika wadhifa huo.

    Katika kile kinachotajwa kuwa mabadiliko makubwa ya kisiasa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960, zaidi ya nusu ya mawaziri waliokuwa chini ya waziri mkuu wa zamani Bi. Theresa May wameondolewa kwenye nyadhifa zao ama kujiuzulu.

    Wakati Johnson akitekeleza hatua hiyo, maelfu ya watu walikusanyika mbele ya jengo la ofisi za waziri mkuu huyo katika Mtaa wa Downing wakipinga uteuzi huo, hatua iliyowalazimu polisi kuweka kizuizi kutowaruhusu waandamanaji hao kuingia kwenye ofisi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako