• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Bondia UDadashev ameaga dunia baada ya kupigwa na kusababishiwa majeraha makubwa kwenye Ubongo

    (GMT+08:00) 2019-07-25 09:37:27

    Kuna wakati unasema michezo mingine ni hatari, Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev amefariki baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo. Dadashev mwenye miaka 28, alishindwa kutembea mwenyewe baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu na kukimbizwa hospitali.

    Madaktari waligundua damu imeivuja kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji wa haraka, lakini alifikwa na umauti Jumanne.

    Wakati huo huo, mabondia wawili ambao wamekuwa wakifanya vizuri miaka ya hivi karibuni Floyd Mayweather na Manny Pacquiao, wameonesha kutofautiana huku kila mmoja akivimba juu ya mwenzake.

    Tofauti hizo wamezionesha kupitia mitandao ya kijamii, baada ya Mayweather kulalamika kuwa kila Pacquiao anapokuwa anafanya jambo lake lazima jina lake litajwe, kitu ambacho amedai ni kumpa umaarufu bondia huyo raia wa Ufilipino.

    Pacquiao na Mayweather walikutana Mei 2, 2015 ambapo Floyd Mayweather aliibuka mshindi kwa pointi ambapo majaji watatu walitoa pointi hizi 118–110, 116–112, 116–112.

    Ugomvi huu wa kwenye mitandao unatafsiriwa kama kichocheo cha wawili hao kurejea ulingoni, kitu ambacho kimekuwa kikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ngumi duniani

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako